Umri wa Miss Tanzania wazua mjadala
Alipotangazwa
mshindi, Miss Tanzania 2014, Sitti, ambaye ni binti wa mbunge wa jimbo
la Temeke jijini Dar es Salaam, alivikwa taji na mtangulizi wake
Happyness Watimanywa, Miss Tanzania 2013.
Kufikia taji hilo la
Miss Tanzania,2014 Bi Sitti ni mshindi wa mara ya ishirini tangu
mashindano hayo yaanze tena nchini humo mwaka 1994. Kabla ya taji hilo,
Bi Sitti alishinda mataji mawili likiwemo la Miss Chang'ombe na Miss
Temeke yote ya mwaka 2014.Pia ataiwakilisha Tanzania katika shindano la Miss World 2015.
Warembo 30 waliingia katika kinyang'anyiro cha Miss Tanzania 2014.
Mara baada ya kutwaa taji hilo kumeibuka utata juu ya umri wa Miss Tanzania 2014.
Habari zimezagaa katika mitandao ya kijamii, ambapo anatuhumiwa kudanganya umri wake. Kuna taarifa zinasema Bi Sitti alitaja kuwa ana umri wa miaka 18, jambo linalobishaniwa.
Lakini ukweli utajulikana Jumanne tarehe 21 Oktoba 2014, ambapo waandaji rasmi wa mashindano ya urembo ya Miss Tanzania, Lino International wameahidi kulitolea ufafanuzi suala hilo.
Je umri halali unaotakiwa mrembo anayeshiriki mashindano hayo ni miaka mingapi?
No comments:
Post a Comment