Mwakilishi
wa Shirika la Umoja wa Mataifa, Wanawake, Anna Collins akitoa hotuba
yake wakati akifungua warsha ya siku moja kuhusu Malengo ya Milenia kwa
washiriki mbalimbali na kwa kiasi ngani Tanzania imeweza kufikia malengo
hayo.iliofanyika Makao Makuu ya Taasisi ya Uchumi na Utafiti wa Kijamii
nchini (ESRF) Oktoba 27, 2014 jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Programu kutoka Taasisi ya…
Mwakilishi
wa Shirika la Umoja wa Mataifa, Wanawake, Anna Collins akitoa hotuba
yake wakati akifungua warsha ya siku moja kuhusu Malengo ya Milenia kwa
washiriki mbalimbali na kwa kiasi ngani Tanzania imeweza kufikia malengo
hayo.iliofanyika Makao Makuu ya Taasisi ya Uchumi na Utafiti wa Kijamii
nchini (ESRF) Oktoba 27, 2014 jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi
wa Programu kutoka Taasisi ya Uchumi na Utafiti wa Kijamii nchini
(ESRF) Dkt Tausi Kida akitoa mada juu ya umuhimu wa kutafuta rasilimali
za kutosha katika kufikia malengo ya milenia hasa kwa nchini
zinazoendelea.
Mkurugenzi
wa Idara Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Celestine Mushy akizungumza
kwenye warsha ya siku moja kuhusu Malengo ya Milenia kwa washiriki
mbalimbali na kwa kiasi ngani Tanzania imeweza kufikia malengo hayo.
Mhadhiri
wa kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dkt Osward Mashindano
akifafanua umuhimu wa kuwashirikisha wananchi wa ngazi ya chini kuhusu
maswala ya malengo ya milenia ili yaweze kufikiwa kwa urahisi zaidi.
Mdau akichangia mada yake.
Wadau wakifurahia jambo wakati ya warsha hiyo.
Wadau mbalimbali walioudhuria wakifuatilia mada mbalimbali.

Na Mwandishi wetu
SERIKALI ya Tanzania imekataa rasmi kutambua ndoa za jinsia moja (ushoga) kama moja ya agenda za maendeleo katika malengo ya milenia 2015 mpaka 2030 katika mkutano wa Umoja wa Mataifa.
Akizungumza jijini Dar es Salaam kwenye mkutano wa majadiliano ya malengo ya milenia yanayotazamiwa kumalizika mwakani na kuanza malengo mapya, Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Celestine Mushy amesema serikali ya Tanzania imekataa kutambua ushoga kama moja ya agenda za maendeleo.
“tunatambua haki za binadamu, usawa wa kijinsia kati ya wanaume na wanawake na hata katiba yetu pendekezwa imetoa haki za sawa kati ya wanaume na wanawake lakini katika swala la kutambua ndoa za jinsia moja hilo tumekataa,” amesema Balozi Mushy
Amesema kwamba tumewaambia nchi zilizoendelea na wahisani wa maendeleo katika Umoja wa Mataifa kwamba swala la ndoa za jinsia moja (ushoga) si agenda ya watanzania na si agenda ya maendeleo.
“Watanzania na Afrika kwa ujumla inataka malengo ya millennia na haki za binadamu zizifike mahali kuwadharirisha watu kutoka bara hili kwa kuruhusu mambo yanayokwenda kinyume na historia yao, mila na desturi za mwafrika,”aliongeza.
Kwa upande wake, Mhadhiri kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dkt Osward Mashindano amesema kwamba malengo ya milenia kwa kiasi kikubwa yamefikiwa na Tanzania hasa katika upande wa elimu na kupunguza vifo vya wakinamama na watoto wakati wa kujifungua.
“leo tumekutana hapa kuzungumza ni kwa kiasi ngani nchi yetu ya Tanzania imefikia malengo ya milenia na changamoto ni zipi katika malengo mapya ambayo ni 17 badala ya 8 ya awali,” aliongeza
Dkt Mashindano alifafanua kwamba ni lazima sasa serikali kutazama katika Nyanja za ubora katika huduma hizi muhimu kwa jamii baada ya kufikia lengo la kuandikisha watoto wenye umri wa kwenda shule kwa asilimia 85.
Aliongeza kwamba Tanzania na dunia kwa ujumla wameona ni muhimu kuweka agenda ya ubora katika kila agenda za malengo ya milenia kwa nchi zote ambao ni wanachama wa Umoja wa Mataifa.
Dkt Tausi Kida, Mkurugenzi wa Programu wa Taasisi ya Uchumi na Utafiti wa Kijamii, amesema kwamba malengo haya ya milenia ni lazima yaguse maisha ya watu katika ngazi ya chini ili matokeo chanya yaweze kuonekana kwenye jamii
Amesema kwamba ni lazima nchi zilizoendelea ziweke mkazo katika kuhakikisha kwamba nchini zinazoendelea zinajengewa uwezo wa kutafuta fedha za kutimiza malengo ya milenia.
No comments:
Post a Comment