
Mbunge wa Mbinga Magharibi John Komba, leo Novemba 6 katika kikao cha Bunge amezungumzia mambo mawili ;-
1- Kuhusu kauli ya Mbunge Peter Msigwa juu ya Katibu mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana; “..kwa
kuanza kwanza ni.. sikupenda sana kwa hotuba aliyoitoa mwenzetu Msigwa
jana kuhusu katibu wetu mkuu Kinana wa CCM.. nataka nimuhakikishie
Msigwa.. kati ya makatibu wakuu tuliowapata katika Chama cha
Mapinduzi..waliokifanyia vizuri chama chetu cha mapinduzi… Kinana ni
miongoni mwao na ndio tishio la upinzani kwa sasa hivi.. Kwa hiyo
kumuingiza Kinana pale kumletea maneno ambayo hajayasema.. ni kiwewe tuu
cha buree cha bure.. Kinana yupo pale kuwaondoeni nyie mnaosema
mtachukua nchi…”—Komba
2- Kuhusu alichofanyiwa Jaji Warioba; “..
Pili nitoe pole kwa mzee Warioba.. juzi yale yaliyompata pale siyo
jambo jema.. na yeye anasema kwamba hayajawahi kuona tangu uhuru..
lakini angesikia ushauri wangu wakati ule wa Bunge la Katiba haya
yasingetokea.. akae tuu pembeni .. aache mjadala wao uendelee kama
kawaida na utaratibu uende kama kawaida yeye alimaliza kazi yake..
wengine wafanye kazi yao na katiba hii mwisho ipatikane nzuri..
ukiingilia ingilia hayo ndiyo yatakayokupata.. mzee pumzika tuu…”– Komba
No comments:
Post a Comment