
Mauzauza? Katika hali ya kushangaza, mwigizaji wa Kundi la Vituko Show linalorusha vipindi vyake kwenye Runinga ya Channel Ten, Jasmini Emiry anadaiwa kuzua timbwili kanisani na kusababisha tafrani madhabauni ikisemekana ni mapepo.
Tukio hilo lililoshuhudiwa na…

Mauzauza? Katika hali ya kushangaza, mwigizaji wa Kundi la Vituko Show linalorusha vipindi vyake kwenye Runinga ya Channel Ten, Jasmini Emiry anadaiwa kuzua timbwili kanisani na kusababisha tafrani madhabauni ikisemekana ni mapepo.
Tukio hilo lililoshuhudiwa na mwanahabari
wetu lilijiri kwenye Kanisa Kuu la Mtakatifu Patriki mjini hapa,
mwishoni mwa wiki iliyopita, wakati wa kuaga mwili wa msanii mwenzake,
Shirley Edward almaarufu Sherry Magali.
Awali, kabla ya zoezi la kuaga mwili wa
marehemu, Jasmini, akiwa benchi la mwisho nyuma sambamba na wasanii
wenzake akiwemo Asha Boko na mke wa Mzee Majuto, Rehema Majuto,
alionekana mwenye simanzi kupita kiasi.
Ulipofika muda wa kuaga, Jasmini
alipomaliza kulizunguka jeneza lililobeba mwili wa Sherry mbele ya
madhabahu, alianguka na kuanza kurusha mateke kama punda huku
akizungumza maneno yasiyoeleweka.
Baada ya kuona hivyo, baadhi ya wasanii wa
Bongo Movies mjini hapa wakiongozwa na Chediel Senzighe walimbeba msanii
huyo na kumtoa nje huku akiwapiga na kuzua tafrani ya aina yake.
Alipofikishwa nje, Jasmini alilala kwenye tairi la gari Toyota
Coaster akitaka limkanyage afe na alipotoka hapo alikimbilia ofisini kwa
paroko na kujilaza kwenye kiti ambapo wasanii wenzake walimkamata na
kuondoka naye kwenye Coaster kisha kwenda kuzika Makaburi ya Kola mjini
hapa.
No comments:
Post a Comment