
Mastaa wa filamu kutoka Nigeria Bob
Manuel Udokwu na Tony One Week Muonago wanaendelea kuzungumziwa sio kwa
sababu wamejiingiza kwenye siasa, bali kinachozungumziwa ni kitendo cha
wao kugombea nafasi hiyo katika jimbo moja kitu ambacho kimeanza
kuvutia hisia za watu wengi.

Bob Manuel Udokwu (kushoto) na Tony One Week, waigizaji wa Nollywood waliojitosa kugombea katika Jimbo la Anambra.
Bob Manuel Udokwu anagombea kupitia
chama cha APGA na Tony One Week Muonagor anagombea kwa tiketi ya ACN
katika jimbo moja la Anambra, Nigeria ambapo uchaguzi mkuu wa nchi hiyo
unatarajiwa kufanyika katikati ya mwaka 2015, ambapo staa mwingine wa
Nollywood ambaye alitangaza kujiingiza kugombea ubunge ni Desmond
Elliot.
Ni halali yako kupata kila stori
inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia
twitter instagram na facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza
>>> twitter Insta Facebook
No comments:
Post a Comment