Mlimani City
ni Shopping Mall ambayo ni maarufu kuliko zote za Tanzania kwa sasa, ni
sehemu ambayo ina mkusanyiko mkubwa wa maduka na migahawa mbalimbali
ambayo kwa miaka ya karibuni imesaidia kuleta mapinduzi ya sehemu za
kufanyia shopping Tanzania.
Na kwa miaka yote kumekua na utaratibu wa kawaida kwamba ukiingia na gari lako
Mlimani City
unapewa tu kadi ambayo unatakiwa kuiacha kwenye geiti wakati ukitoka na
hautoulizwa kitu kingine hata ukilipaki gari lako kuanzia asubuhi mpaka
jioni ila sasa hivi utaratibu umebadilika.

Yeyote anaeingia na gari ni lazima alilipie
Parking
ambayo inalipwa kutokana na muda uliopaki, ukipaki ndani ya dakika 60
hautochajiwa chochote ila dakika 60 zikizidi mpaka dakika 120 utalipia
shilingi 500.
Kwenye dakika 120 (saa mbili) mpaka dakika 180 (saa tatu) utalilipia
gari lako shilingi elfu moja wakati kwa saa tatu mpaka nne utalipia
shilingi elfu moja mia tano na ukizidisha na kufikia saa tano
itaongezeka shilingi mia tano kwa saa moja.

Wakati wa kutoka
Mlimani City
ni lazima ulipie parking kabla ya kutoka na gari lako, utakwenda kwenye
vituo maalum na kuingiza kadi yako pamoja na kiwango unachodaiwa kama
inavyoonekana hapa chini.

Unapenda stori kama hizi zisikupite? ungana na mtu wako
Millard Ayo kwa kubonyeza hapa ili niwe nakutumia moja kwa moja mtu wangu >>>
Twitter InstagramFacebook
No comments:
Post a Comment