
Na stori hii inamhusu sokwe mmoja ambaye
amepewa jina la Zaire, ambaye anafugwa katika bustani moja ya wanyama
London, Uingereza amesherehekea siku yake ya kuzaliwa ambapo ametimiza
miaka 40.
Na kama haitoshi, party yake ilikuwa poa
kama ambazo huwa tumezoea kufanya binadamu, ametengenezewa keki ya
nguvu katika sherehe hiyo na moja ya mabingwa wa kutengeneza keki za
sherehe, Richard Burr.
Unaambiwa sokwe huyu anapendelea vitu
kama jelly zisizo na sukari, apples, na karoti hivyo mwandaaji wa keki
alijikuta na jukumu la kuhakikisha anamuandalia keki itakayomfurahisha
Zaire.
Hizi ni picha za Sokwe huyo akijiachia na keki akisherehekea.
Ni halali yako kupata kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia twitter instagram na facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>> twitter Insta Facebo
No comments:
Post a Comment