MTIFUANO! Tamasha la Serengeti Fiesta 2014 limepita lakini nyuma yake limeacha vita nzito iliyowahusisha mafahari wawili, Nasibu Abdul ‘Diamond’ na Ali Kiba huku waandaaji wa tamasha hilo, Clouds FM wakisigana na Times FM kumgombea msanii wa Nigeria, David Adedeji Adeleke ‘Davido’, Risasi Mchanganyiko linakupa mchongo kamili.

Stori: Erick Evarist, Musa Mateja na Chande Abdallah
MTIFUANO! Tamasha la Serengeti Fiesta 2014 limepita lakini nyuma yake limeacha vita nzito iliyowahusisha mafahari wawili, Nasibu Abdul ‘Diamond’ na Ali Kiba huku waandaaji wa tamasha hilo, Clouds FM wakisigana na Times FM kumgombea msanii wa Nigeria, David Adedeji Adeleke ‘Davido’, Risasi Mchanganyiko linakupa mchongo kamili.
TIFU LILIVYOKUWA
Kwenye shoo hiyo iliyofanyika wikiendi iliyopita katika Viwanja vya Leaders Club, Kinondoni jijini Dar, mashabiki wanaodaiwa kuwa ni wafuasi wa Ali Kiba (Team Kiba), walipiga kelele za ‘buuu’ pale alipopanda Diamond kutumbuiza ili kumharibia.
Staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’.
CHANZO CHANENAChanzo makini kimedai kuwa, vurugu hizo hazikutokea kwa bahati mbaya bali zilipangwa na wafuasi wa Kiba ambapo inasemekana ziliandaliwa gari aina ya Toyota-Costa zipatazo 25 zilizokuwa zimejaa watu na kwenda kuwamwaga viwanjani hapo kwa shughuli mbili muhimu; kuzomea na kuhamasisha wengine wazomee pindi Diamond atakapopanda jukwaani.
Msanii wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’ akifanya shoo na Davido wa Nigeria.
“Ishu ilipangwa, Team Kiba waliibuka na Costa kama 25 hivi,
wakajipanga katika maeneo tofauti ya uwanja huo lakini zaidi walikaa
karibu na jukwaa ili kuweza kutimiza vizuri azma yao ya kuharibu pindi
Diamond atakapokuwa akitumbuiza,” kilidai chanzo hicho.WALIFANIKIWA?
Kwa namna moja mashabiki hao walionekana kufanikiwa kwani waliweza kuwashawishi watu wengi wazomee kiasi cha kumfanya Diamond ashtukie na kuamua kutamka hadharani: “Jamani kuna uhuni unaendelea hapa.”
Mkurugenzi wa Times Fm Rehure Nyaulawa
No comments:
Post a Comment