Je nyama hii ndio chanzo cha Ebola?

Nyama wa wanyama wa msituni ndio
inaaminika kuwa chanzo cha mlipuko wa Ugonjwa wa Ebola ambao umekuwa
janga kwa mataifa kadhaa ya Afrika Magharibi na kwa ulimwengu wote.
Familia ya Mwathiriwa wa kwanza wa Ugonjwa huo iliwinda Popo ambao huwa na virusi vya Ebola.Lakini katika baadhi ya wanyama hawa huwa wamebeba magonjwa hatari.
Kama Popo huwa wamebeba virusi aina tofauti ambavyo ni hatari kwa mwili wa binadamu huku baadhi ya Popo wanaokula matunda wakiwa na virusi vya Ebola.
Kwa wanyama hao kama kwa binadamu virusi hivyo vinaweza kuwa hatari.
Lakini Popo wanaweza wasiathirike sana.
Kwa hivyo inakuwa rahisi kwao kubeba virusi hivyo bila ya kuathirika kwa vyovyote

No comments:
Post a Comment