
Baadhi ya viongozi wakubwa duniani ikiwemo Marais, Viongozi wa kidini na wengineo wamekuwa na utaratibu wa kutumia huduma za mitandao ya kijamii na simu za mkononi kuwasiliana na watu.
Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta ni moja ya marais ambao wamekuwa wakitajwa kutumia sana mitandao ya kijamii ikiwemo Twitter.
Huenda usiamini alichokifanya Rais Uhuru
Kenyatta, stori ni kwamba baada ya kutumiwa message na Anita Lipesa
ambaye alikwama shilingi milioni tatu na laki tano za Kenya kwa ajili ya
kutoa mwili wa dada yake aliyefariki kutoka chumba cha kuhifadhia
maiti.
Anita amesema baada ya jitihada za
kuchangisha michango kushindikana aliamua kumtumia ujumbe kwa Rais
Kenyatta ingawa hakuwa na tumaini lolote kujibiwa, dakika 30 baada ya
kutuma message hiyo Kenyatta alimpigia simu dada huyo ambaye hakuamini
kama Rais angeweza kufanya hivyo.
Dada huyo anasema baada ya kumwelezea
Rais kilichotokea alipata msaada wa kuutoa mwili wa dada yake huyo na
kwenda kufanya mazishi.
Ni halali yako kupata kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari
kukutumia wakati wowote kupitia twitter instagram na facebook ukijiunga
na mimi kwa kubonyeza >>> twitter Insta Facebook
No comments:
Post a Comment