Stori: Mwandishi Wetu HUKU
mwenyewe akikanusha vikali kwamba hatumii, nyota wa muziki wa Injili
Bongo, Rose Muhando bado anaandamwa na madai mazito kwamba anatumia
madawa ya kulevya ‘unga’ yanayomfanya kuwa hoi kiasi cha kushindwa
kutokea kwenye matamasha mbalimbali anayolipwa fedha, Risasi Jumatano
linateremka nayo.
Nyota wa muziki wa Injili Bongo, Rose Muhando.
Kwa mujibu wa vyanzo, Rose anadaiwa kutumia unga kiasi kwamba, baada
ya matumizi hujikuta akishindwa kufanya jambo lolote lile la…
Stori: Mwandishi Wetu HUKU
mwenyewe akikanusha vikali kwamba hatumii, nyota wa muziki wa Injili
Bongo, Rose Muhando bado anaandamwa na madai mazito kwamba anatumia
madawa ya kulevya ‘unga’ yanayomfanya kuwa hoi kiasi cha kushindwa
kutokea kwenye matamasha mbalimbali anayolipwa fedha, Risasi Jumatano
linateremka nayo.
Nyota wa muziki wa Injili Bongo, Rose Muhando.
Kwa mujibu wa vyanzo, Rose anadaiwa kutumia unga kiasi kwamba, baada
ya matumizi hujikuta akishindwa kufanya jambo lolote lile la kujitafutia
mkate wake wa kila siku na ndiyo maana amekuwa akikwaa skendo za
kupokea fedha za shoo halafu hatokei tu!
WATOA MADAI
Hivi
karibuni, akina mama watatu walifika kwenye Ofisi za Global Publisheers
na kumtolea madai Rose kuhusu tuhuma zanazomwandama kwamba amekuwa
akiingia mitini na fedha za watu wanaomwita kwenye matamasha ya nyimbo
za Injili.
“Sisi
tunavyojua, Rose anatumia madawa, wengine wanasema unga wengine
wanasema sijui nini huko. Sasa akishatumia hayo madawa huwa yanamfanya
awe kama amelewa na kushindwa kufanya lolote.
“Huwa anafika hatua
anashinda kitandani amelala tu na hawezi kutoka, ndiyo maana mtu anaweza
kumpa pesa asitokee kuimba kwa sababu anashindwa kutoka ndani kwake.
“Kwa hiyo jamani, si suala la kumwandika tu
kwamba anaingia mitini na fedha za watu bali mumsaidie Rose kama kweli
mnampenda, sisi wenyewe tunamwombea kwa Mungu kila siku,” alisema mama
mmoja kati ya hao waliofika lakini bila kutaja majina yao.
MADAI SUGU Madai ya kwamba, Rose anatumia madawa
ni ya siku nyingi, wengi wamekuwa wakisema wana uhakika, wengine
wanasema wanasikiasikia tu lakini hawana uhakika.
Mratibu wa Tamasha la Pasaka, Alex Msama.
Magazeti ya Global (Ijumaa Wikienda, Uwazi, Risasi Jumatano, Amani,
Ijumaa na Risasi Jumamosi) yameshapokea madai hayo kwa muda mrefu lakini
kilichokuwa kikifanyika ni kuendelea kumchunguza msanii huyo kuhusu
madai hayo.
RISASI LAINGIA KAZINI KUCHUNGUZA Kufuatia madai
ya akina mama hao waliojitambulisha ni waumini wa kutoka katika kanisa
moja la kilokole jijini Dar, gazeti hili liliamua kuingia kazini kufanya
uchunguzi ili kubaini ukweli au uongo wa madai hayo.
WATU WA KARIBU NA ROSE Mtu wa kwanza kumtafuta
ambaye gazeti hili liliamini kwamba anaweza kujua chochote kuhusu madai
hayo ni mratibu wa Tamasha la Pasaka linalofanyika kila mwaka kwenye
baadhi ya mikoa, Alex Msama.
Msama: “Mimi siwezi kusema ni kweli kwani sijawahi kumwona akitumia wala sijui kama ameathirika.”
Risasi Jumatano likamsaka Katibu wa Chama cha Waimba
Injili Tanzania (Chawaita), Stela Joel: “Mimi sijui, kama unasema kuna
watu wamekuja ofisini kwenu na kutoa madai hayo, basi wamwombee. Lakini
tutachunguza.”
MCHUNGAJI Risasi Jumatano pia lilibahatika
kuzungumza na mchungaji mmoja (jina tunalo) ambaye alisema ameshawahi
kusikia taarifa hizo akamuuliza Rose lakini alimkatalia kuwa si madai ya
kweli.
“Ila ninachojua mimi ni kwamba, Rose amekuwa akitumia dawa f’lani
(akazitaja jina). Hizi ni dawa zinazopatikana kwa njia ya sindano. Mara
nyingi mtu akiwa hajiwezi kwa maana ya kushindwa kufanya kazi anachomwa
hizi zinampa nguvu.
“Niliwahi kusikia kwamba, kuna daktari mmoja katika Hospitali ya Mkoa
wa Dodoma (akamtaja jina). Huyu ndiye aliyekuwa akimchoma sindano zenye
dawa hizo Rose pale mwili unapokuwa dhaifu.
Baadhi ya madawa yaliyowahi kukamatwa.
“Ila madhara yake sasa, dawa ikiwa imekwisha mwilini, mtu anakuwa
mlegevu, anahisi kizunguzungu au kulalalala, kutokwa jasho jingi na
kuhisi anaumwa kiasi kwamba ukimwona unaweza kusema ni teja. Ni dawa
ghali sana kwa dozi moja, nadhani ni shilingi laki sita,” alisema
mchungaji huyo.
Akaongeza: “Nasikia Rose amefika mahali huwa
anajichoma mwenyewe akipata dozi. Kwa hiyo kwa suala la kubwia unga
nadhani alilikanusha.”
ROSE MWENYEWE SASA Risasi Jumatano,
juzi lilimpigia simu Rose lakini hakupokea hata baada ya kurudia
kumpigia mara kadhaa. Likamtumia meseji na kumsomea mashitaka yote,
akajibu:
“Samahani sana nawaomba mnipumzishe kuniandika...najua ni nani na kwa
nini ananitenda hivyo, ni kwa sababu anataka kunitumia kwa faida yake
na ni mtu hatari sana kwangu na kwa taifa zima.
“Mtu huyo anafanya haya ili kuniziba mdomo kwani najua siri zake nyingi na nzito, nashindwa kusema ataniua.”
Hata hivyo, Rose alipotakiwa kumtaja kwa jina mtu huyo ambaye Risasi Jumatano halimjui, alikataa katakata akisema anaogopa!