Imekua
stori namba 1 kwa mwezi wa October 2014 inayomuhusu msanii kwenye
familia ya bongofleva iliyoandikwa au kuripotiwa na kila aina ya chombo
cha habari kuanzia TV, Magazeti na hata mitandaoni.Chidi Benz alikamatwa na dawa za kulevya kete 14 pamoja na bangi kwenye uwanja wa ndege Dar es salaam akielekea Mbeya kwenye show aliyokua anatakiwa kuifanya kesho yake lakini ilishindikana kutokea baada ya kukamatwa na Polisi, baadae akafikishwa Mahakamani na sasa yuko nje kwa dhamana.
Alipohojiwa na So so fresh ya CloudsFM inayoongozwa na Dj Fetty, haya ni mambo sita aliyoyazungumza ambapo sentensi mbili ni zake na Tour ya Profesa Jay na nyingine nne ni ishu yake ya kukamatwa Airport.
Kuhusu Tour aliyoifanya na Profesa Jay >>>
‘Ilikua poa sana tumezunguka Dodoma, Morogoro na vitongoji vyake…
tumekumbuka zamani tulivyokua tukizunguka kijiji baada ya kijiji,
tumefanya kazi vizuri sana na Profesa amekua akinisifia kwa kusema
nakuona uko poa afya yako iko poa’‘Aliniambia by the way nilikua nataka kama unaendelea kuvuta, naona mambo ya kuvutavuta umeachana nayo, tunakaa karibia muda wote tunazunguka wote hata kunywa nimesimama kwa hiyo sasa hivi sio tena muda wa kujielezea oooh navuta, oooh sivuti oooh nakunywa…. naendelea na maisha yangu kama kawaida’
Kuhusu kukamatwa Aiport
na dawa za kulevya Benz amesema >>> ‘Sikuwaambia Polisi kwamba
natumia dawa walizonikamata nazo, niliwaambia dawa nilizokua nazo
lazima nilikua nimechanganya kipindi nilikua nazitumia nilikua
nafichaficha kwenye nguo zangu, enzi zile nilikua naficha dawa kwa
kuziweka hivyo nikiwa sitaki mtu ajue’‘Shetta aliponipigia simu ya fasta ili tusafiri kutoka Dar es salaam kwa ndege mpaka Mbeya nikalichukua tu shati na kulivaa na jeans na nilivyofika Airport nikawa namtania tu Shetta namwambia mdogo wangu nimebeba mambo kibao, mabegi yamejaa yote ila sina viatu wala nguo, imagine nafika pale nasachiwa nakutwa na dawa kwenye mfuko wa shati kushoto… sio kama nimeficha au nini’
‘Sio
kitu nilikua nimepanga, sio kitu nilikua nimeplan…. mi mwenyewe
nimejisachi nikakutwa nayo, sijakamatwa…… mimi nimezitoa…. natoa hivi
nakutana na vidude kama kadhaa naviona tu mkononi hapa, jamaa akaviona
akaniambia hii nini? nikamwambia hii dawa lakini sijui imekuaje na mimi
pale kidogo kibinadamu akili ilikua imeniruka kugundua ile ni dawa na
nimeitoa mwenyewe’‘Kama nilipigwa na butwaa hivi nikajaribu kuomba jamaa nikawaambia bwana sorry kuna time nilikua natumia hizi vitu nikaachana nazo, so kama mnaweza kunielewa mkanisamehe wakasema hakuna….. wakasachi kila begi na hawakukuta kitu kingine’ – Chidi Benz
Kesi ya Chidi Benz imepangwa tena November 11 2014.
Umeyaamini maneno ya Chidi Benz kwa asilimia ngapi? niachie comment yako hapa chini mtu wangu
Unataka chochote kinachonifikia kisikupite? ungana na mimi hapa ili niwe nakutumia moja kwa moja >>> Twitter
No comments:
Post a Comment