Thursday, 6 November 2014

Magazeti ya leo Nov 5 2014 Udaku, Michezo na Hardnews

.
.
Kama kawaida millardayo.com inakupa vichwa vya habari vya magazeti yote ya kila siku. Leo pia kuna headline mpya kwenye magazeti mbalimbali. Chukua muda wako kupitia kila kilichoandikwa kwenye kurasa za mbele za magazeti ya leo.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
DSC05272
.
.
.
.
.
.
DSC05276
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
Ni halali yako kupata kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia twitter instagram na facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>> twitter Insta Facebook

Stori 7 Hot za Magazeti ya Tanzania leo November 6 2014

Hotnews 12 

HABARILEO
Baraza la Mtihani la Taifa NECTA limetangaza matokeo ya darasa la Saba yanaonyesha kuwa ufaulu umeongezeka kutoka asilimia 6.38 huku Mikoa ya kanda ya Ziwa ikitoa shule nane kati ya kumi bora kitaifa huku shule nyingine mbili zinazokamilisha ufaulu huo zinatoka Dar es Salaam na Kilimanjaro.
Katibu Mtendaji wa NECTA Charles Msonde alisema zaidi ya wanafunzi laki nne kati ya laki nane waliofanya mtihani wamepata alama za juu za 100 na zaidi kati ya alama250 ambayo ni sawa na asilimia56.99 ambapo mwaka jana ufaulu ulikua kwa  asilimia50.61.
Hata hivyo alisema wanafunzi zaidi ya laki tatu wamefeli mtihani huo kwa kupata alamaD na E  huku wasichana wakifanya vizuri kuliko wanaume.
Aidha alisema takwimu za matokeo zinaonyesha ufaulu katika masomo yote umepanda kwa asilimia kati ya 0.64 hadi 8.94 ikilinganishwa na mwaka jana huku watahaniwa wakifaulu zaidi somo la kiswahili.
HABARILEO
Bunge limeelezwa kuwa deni la walimu linalodaiwa Serikali limeshuka hadi kufikia bilioni4 tu kutokana na mfumo mzuri unaolipwa na Wizara ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa TAMISEMI
Akijibu swali bungeni,la Mbunge wa viti maalumDiana Chololo kuhusu madai ya walimu,Naibu Waziri wa Fedha Mwigulu Nchemba alisema kwa sasa kiwango hicho kimeshuka hadi kufikia bilioni4 kutoka zaidi ya bilioni60 ambazo zilikua zikidaiwa.
Alisema hatua hiyo inadhihirisha nia njema ya Serikali ya kulipa madeni yote ya walimu kwa lengo la kuboresha maisha yao na hasa baada ya kuboreshwa kwa mfumo wa ulipwaji ambao kwa sasa hautawezesha tena deni hilo kukua.
Alisema lengo la serikali la kulipa moja kwa moja katika akaunti ni kuepuka mishahara hewa inayolipwa kwa watumishi wasiostahili.
MWANANCHI
Wizara ya Maliasili imesema tatizo la ujangili limelisababishia Taifa hasara kubwa kiuchumi inaofikia kiasi cha bilioni1.8.
Naibu waziri wa maliasili Mahamud Mgimwa alieleza hasara hiyo ilikua katika kipindi cha mwaka 2013/14 ambacho wanyamapori205 wa aina mbalimbali waliuawa.
Jambo jingine alisema kuwa ni matumizi makubwa ya rasilimali watu,fedha na muda katika kupambana na ujangil kwenye mbuga mbalimbali za wanyamapori.
Kuhusu doria alisema katika kipindi hicho ilifanyika ndani na nje ya maeneo yaliyohifadhiwa ikiwemo kuwakamata majangili998 waliofikishwa katika vyombo vya sheria huku wengine wakilipa zaidi ya milioni256 kama fidia.
MWANANCHI
Watu wasiofahamika wamemuua kwa kumkatakata mapanga na kisha kumnyofoa sehemu za siri mwanamke mmoja Hollo Machibula mwenye umri wa miaka54 Wilani Geita.
Diwani wa kata ya Bikandwe Henry Alphonce alisema mwanamke huyo alivamiwa na watu hao majira ya saa5 usiku wakati amelala na kuanza kumkatakata mapanga.
Alisema mwanamke huyo alikua akiishi na binti yake mwenye umri wa miaka25 ambapo wauaji hao walimlazimisha kuingia chini ya uvungu wa kitanda kabla ya kuanza kumshambulia mama yake.
Akisimulia tukio hilo binti huyo alisema alishuhudia mama yake akichinjwa na watu hao kisha kunyofolewa sehemu zake za siri walizotoweka nazo wauaji hao.
Chanzo kinadai mauaji hayo huenda yamesababishwa na ugomvi kati ya marehemu na mumewe ambao wlaikua na ugomvi mkubwa wa kifamilia.
NIPASHE
Mke wa Waziri mkuu Tunu Pinda amesema bado hajashirikishwa na mume wake Mizengo Pinda kuhusu nia ya kiongozi huyo wa nchi kuwania nafasi ya urais katika uchaguzi mkuu ujao mwakani.
Alisema mume wake bado hajatangaza nia hiyo ya kuwania nafasi hiyo kubwa kwani hajawah kukaa na familia yake na kuweka bayana juu ya nia yake ya kutaka urais.
“Mume wangu bado hajatangaza rasmi kuwania uraisi,mimi kama mke wake hajaniambia na hata watoto wake hajawashirikisha,na sisi kama Watanzania tunatakiwa kufahamu uraisi ni baraka toka kwa Mungu hivyo kama atafanya hivyo itakua ni jambo jema”alisema Tunu.
Alisema na hata kama atatangaza kuwania nafasi hiyo na hatimaye kukosa hatajisikia vibaya kwani anaamini nafasi hiyo Mungu ndiye anayepanga nani ataongoza nchi hii baada ya utawala wa rais Kikwete.
JAMBOLEO
Ukata wa fedha ambao umevikumba vikao vya kamati za bunge umesababisha Naibu Spika Job Ndugai kuiomba Wizara ya Fedha kushughulikia posho za wabunge ili walipwe kwa ajili ya vikao vinavyoendelea.
Ndugai alitoa kauli hiyo Bungeni wakati naibu Waziri wa fedha Mwigulu Nchemba akijibu maswali ya wabunge hao kuhusu Wizara hiyo kwamba ina majibu mazuri na uhakika.
Baadhi ya wabunge hao walionekana kuwa na wasiwasi kuhusu ni lini watalipwa fedha zao huku wakisema hawaielewi Wizara ya fedha ina mpango gani nao mpaka sasa.
MTANZANIA
Shirika la bima la Taifa NIC limekana kudaiwa deni la milioni8.7 na hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) ambalo limesababisha kukatwa kwa huduma ya matibabu kwa mkopo dhidi ya wafanyakazi wake.
Meneja wa Pensheni na Bima wa shirika hilo Henry Mwalwisi alisema NIC haijapokea taarifa yoyote kutoka Muhimbili kuhusu deni hilo na kwamba taarifa hizo alizisoma kutoka kwenye vyombo vya habari.
Alisema baada ya Taarifa hizo NIC ililazimika kumtuma daktari kwenda kuhakikisha katika ubao wa matangazo wa hospitali hiyo na kukuta ni kweli wanadaiwa deni hilo.
“Alikuja na kutuletea deni hilo la milioni8.7 lakini ninachofahamu mimi  tulikua tumelipa na kubakiza milioni2.5 katika deni hilo na ofisi ya muhasibu imeidhinisha deni hilo na kwamba litaingizwa kwenye akaunti ya Muhimbili siku yoyote kuanzia sasa,tunashangazwa na kiasi hicho kikubwa walichotaja”alisema.
Ni halali yako kupata kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia twitter instagram na facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>> twitter Insta Facebook

Stori hii inahusu mtu aliyempigia simu Rais kuomba msaada wa fedha kuutoa mwili wa dada yake Mochwari…

news

Baadhi ya viongozi wakubwa duniani ikiwemo Marais, Viongozi wa kidini na wengineo wamekuwa na utaratibu wa kutumia huduma za mitandao ya kijamii na simu za mkononi kuwasiliana na watu.
Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta ni moja ya marais ambao wamekuwa wakitajwa kutumia sana mitandao ya kijamii ikiwemo Twitter.
Huenda usiamini alichokifanya Rais Uhuru Kenyatta, stori ni kwamba baada ya kutumiwa message na Anita Lipesa ambaye alikwama shilingi milioni tatu na laki tano za Kenya kwa ajili ya kutoa mwili wa dada yake aliyefariki kutoka chumba cha kuhifadhia maiti.
Anita amesema baada ya jitihada za kuchangisha michango kushindikana aliamua kumtumia ujumbe kwa Rais Kenyatta ingawa hakuwa na tumaini lolote kujibiwa, dakika 30 baada ya kutuma message hiyo Kenyatta alimpigia simu dada huyo ambaye hakuamini kama Rais angeweza kufanya hivyo.
Ukenyatta
Dada huyo anasema baada ya kumwelezea Rais kilichotokea alipata msaada wa kuutoa mwili wa dada yake huyo na kwenda kufanya mazishi.
Lipesa
Anita (mwenye t-shirt nyeusi) akiwa na familia yake.
Ni halali yako kupata kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia twitter instagram na facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>> twitter Insta Facebook

Inabidi ujue kabisa kwamba ukiingia Mlimani City na gari lako utakutana na hii



M City 4Mlimani City ni Shopping Mall ambayo ni maarufu kuliko zote za Tanzania kwa sasa, ni sehemu ambayo ina mkusanyiko mkubwa wa maduka na migahawa mbalimbali ambayo kwa miaka ya karibuni imesaidia kuleta mapinduzi ya sehemu za kufanyia shopping Tanzania.
Na kwa miaka yote kumekua na utaratibu wa kawaida kwamba ukiingia na gari lako Mlimani City unapewa tu kadi ambayo unatakiwa kuiacha kwenye geiti wakati ukitoka na hautoulizwa kitu kingine hata ukilipaki gari lako kuanzia asubuhi mpaka jioni ila sasa hivi utaratibu umebadilika.
Mlimani City ParkingYeyote anaeingia na gari ni lazima alilipie Parking ambayo inalipwa kutokana na muda uliopaki, ukipaki ndani ya dakika 60 hautochajiwa chochote ila dakika 60 zikizidi mpaka dakika 120 utalipia shilingi 500.
Kwenye dakika 120 (saa mbili) mpaka dakika 180 (saa tatu) utalilipia gari lako shilingi elfu moja wakati kwa saa tatu mpaka nne utalipia shilingi elfu moja mia tano na ukizidisha na kufikia saa tano itaongezeka shilingi mia tano kwa saa moja.
M City 1 Wakati wa kutoka Mlimani City ni lazima ulipie parking kabla ya kutoka na gari lako, utakwenda kwenye vituo maalum na kuingiza kadi yako pamoja na kiwango unachodaiwa kama inavyoonekana hapa chini.
m city 2
m city 3Unapenda stori kama hizi zisikupite? ungana na mtu wako Millard Ayo kwa kubonyeza hapa ili niwe nakutumia moja kwa moja mtu  wangu >>> Twitter InstagramFacebook

Alichokizungumza kapteni Komba kuhusu Mzee Warioba na Kinana…

image-06-11-14-04-17-10
Mbunge wa Mbinga Magharibi John Komba, leo Novemba 6 katika kikao cha Bunge amezungumzia mambo mawili ;-
1- Kuhusu kauli ya Mbunge Peter Msigwa juu ya Katibu mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana; “..kwa kuanza kwanza ni.. sikupenda sana kwa hotuba aliyoitoa mwenzetu Msigwa jana kuhusu katibu wetu mkuu Kinana wa CCM.. nataka nimuhakikishie Msigwa.. kati ya makatibu wakuu tuliowapata katika Chama cha Mapinduzi..waliokifanyia vizuri chama chetu cha mapinduzi… Kinana ni miongoni mwao na ndio tishio la upinzani kwa sasa hivi.. Kwa hiyo kumuingiza Kinana pale kumletea maneno ambayo hajayasema.. ni kiwewe tuu cha buree cha bure.. Kinana yupo pale kuwaondoeni nyie mnaosema mtachukua nchi…”—Komba
Komba2- Kuhusu alichofanyiwa Jaji Warioba; “.. Pili nitoe pole kwa mzee Warioba.. juzi yale yaliyompata pale siyo jambo jema.. na yeye anasema kwamba hayajawahi kuona tangu uhuru.. lakini angesikia ushauri wangu wakati ule wa Bunge la Katiba haya yasingetokea.. akae tuu pembeni .. aache mjadala wao uendelee kama kawaida na utaratibu uende kama kawaida yeye alimaliza kazi yake.. wengine wafanye kazi yao na katiba hii mwisho ipatikane nzuri.. ukiingilia ingilia hayo ndiyo yatakayokupata.. mzee pumzika tuu…”– Komba
Ukitaka kuisikiliza sauti ya Komba akizungumzia hayo leo Novemba 6 kwenye kikao cha Bunge, iko hapa bongyeza play.

Saturday, 1 November 2014

IKO ABONDWA

Stori: Hamida Hassan na Gladness Mallya


STAA wa filamu za Kibongo, Tiko Hassan, hivi karibuni alionja joto ya jiwe baada ya kushushiwa kipigo kizito na hawara wake aliyetajwa kwa jina moja la Ally.
Staa wa filamu za Kibongo, Tiko Hassan akiwa na jeraha la kipigo kutoka kwa hawara yake.
Kwa mujibu wa chanzo makini, siku ya tukio Tiko alikuwa na Ally nyumbani kwake, Mwananyamala ndipo ghafla hali ya hewa ikachafuka baada ya pedeshee mmoja kumpigia simu mwigizaji…
Stori: Hamida Hassan na Gladness Mallya
STAA wa filamu za Kibongo, Tiko Hassan, hivi karibuni alionja joto ya jiwe baada ya kushushiwa kipigo kizito na hawara wake aliyetajwa kwa jina moja la Ally.
Staa wa filamu za Kibongo, Tiko Hassan akiwa na jeraha la kipigo kutoka kwa hawara yake.
Kwa mujibu wa chanzo makini, siku ya tukio Tiko alikuwa na Ally nyumbani kwake, Mwananyamala ndipo ghafla hali ya hewa ikachafuka baada ya pedeshee mmoja kumpigia simu mwigizaji huyo.
“Mzozo ulianzia kwenye simu na huwezi amini amemvunjia simu yake kwani alimpiga kwa sababu alikuwa akiongea na mwanaume mmoja kimahaba na hapo ndipo timbwili lilipoanza,” kilidai chanzo hicho.
Kikazidi kumwaga ubuyu kwamba, wakati kipigo cha ngumi kikiendelea, mwanaume huyo alimrushia chupa Tiko ambayo ilimpasua usoni na kumuacha na jeraha kubwa lakini hakwenda kumshtaki polisi kwa kuwa anampenda sana.
Tiko Hassan akiuguza jeraha lake.
Baada ya habari hizo kutua gazetini, mapaparazi wetu walimtafuta Tiko na kufanikiwa kumpata nyumbani kwao Mbagala ambapo alifunguka:
“Yule ana wivu sana na mimi, huyo mtu aliyenipigia simu simjui na alikuwa akijaribu kunitongoza na mimi nilikuwa nikimkaripia lakini kibao kilinirudia, nikapigwa.
“Nilitibiwa katika Hospitali ya Cam hapa Mbagala, kwa sasa nauguza kidonda nikipona nitajua cha kumfanyia kwani amenifanya niwe na jeraha usoni.”

FUMANIZI LA MWALIMU


Stori: Dustan Shekidele, Morogoro    

KATIKA hali ya kutisha, fumanizi lililoambatana na bonge moja la mtiti linadaiwa kujiri nyumbani kwa mwalimu ‘ticha’ wa Shule ya Msingi ya Mafisa ‘A’, iliyopo Manispaa ya Morogoro mjini hapa aliyefahamika kwa jina la Rosemary Mkoba kisha watu wakachomana visu.

Mume wa mtu, Raphael Bernard (33) aliyechomana visu na mwalimu baada ya fumanizi.
HABARI KAMILI

Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo, msala…
Stori: Dustan Shekidele, Morogoro    
KATIKA hali ya kutisha, fumanizi lililoambatana na bonge moja la mtiti linadaiwa kujiri nyumbani kwa mwalimu ‘ticha’ wa Shule ya Msingi ya Mafisa ‘A’, iliyopo Manispaa ya Morogoro mjini hapa aliyefahamika kwa jina la Rosemary Mkoba kisha watu wakachomana visu.
Mume wa mtu, Raphael Bernard (33) aliyechomana visu na mwalimu baada ya fumanizi.
HABARI KAMILI
Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo, msala huo ulijiri juzikati nyumbani kwa ticha huyo, Kichangani ambapo mwalimu huyo alidaiwa kufumwa na mume wa mtu, Raphael Bernard (33) ambaye ni dereva wa bodaboda.
ILIKUWAJE?
Habari zilidai kwamba mwenye mume amekuwa akimfuatilia mumewe kwa muda mrefu, akagundua huwa anakwenda kujichimbia kwa ticha huyo huku akiacha familia ikilala njaa.
Ilisemekana kuwa, siku ya tukio, mwenye mume, akiwa na ‘jeshi’ lake, alimfuatilia mumewe hadi akamuona akiingia nyumbani kwa hawara wake huyo.
APEWA MUDA AVUTE PUMZI
Ikazidi kudaiwa kwamba baada ya kuhakikisha jamaa amelala kwa ticha huyo, mwanamke huyo na ‘skwadi’ yake waliondoka, asubuhi iliyofuata mishale ya saa 1:04 wakatia timu na kulianzisha timbwili huku mke huyo akidaiwa kumtishia ticha kuwa akipata ujauzito atazaa kwa mdomo.
Bw. Raphael Bernard akiuguza majeraha hospitalini.
Habari zinadai kuwa, baada ya mke huyo na timu yake kuondoka, ticha huyo alimuwakia Raphael kwamba kumbe ana mke, kwa nini hakuwahi kumwambia? Ugomvi mwingine ukazuka hapo.
MASHUHUDA SASA
Nao mashuhuda ambao ni majirani wa mwalimu huyo, Juma Hamis na Joyce Joseph, walipozungumza na paparazi wetu walisema siku hiyo walisikia vurugu kutoka ndani kwa mwalimu ambapo walikwenda kushuhudia.
Walisema walimkuta mwanaume huyo akipigana na ticha ambaye alikuwa akiendelea kulalamika kufichwa suala la mwanaume wake kuwa na mke.
WACHOMANA VISU
“Unaambiwa mzozo huo ulipamba moto, maana yule mke aliyeondoka alidai amemfumania mumewe, mwalimu naye akadai alikuwa hajui.
“Katika purukushani hiyo huku wakipigana wao kwa wao ndipo wakachomana visu. Yaani mwanaume alijeruhiwa vibaya mno.
Mwalimu ‘ticha’ wa Shule ya Msingi ya Mafisa ‘A’ aliyechomana visu na Bw. Raphael Bernard.
“Mwanaume alichomwa kisu utumbo ukatoka nje na kama siyo polisi kufika na kukimbizwa hospitalini, sasa hivi tungekuwa tunaimba ‘Parapanda Italia….Parapanda…’ kwani hali ilikuwa mbaya sana,” alisema Joyce kwa masikitiko.
HOSPITALINI
Baada ya kuzungumza na majirani na mashuhuda wa tukio hilo, mwanahabari wetu alitia gia kwenye pikipiki yake aina ya ‘boksa’ hadi Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro.
Mwandishi wetu alizungumza na Kaimu Mganga Mfawidhi, Dk. Francis Semwene ambaye alikiri kuwapokea majeruhi hao.
“Mwanaume alikuwa amepasuka tumboni hivyo tunaendelea kumpa matibabu, yupo wodi namba moja na mwanamke ambaye naye amechomwa visu sehemu mbalimbali za mwili wake, naye tunaendelea kumpatia matibabu,” alisema Dk. Semwene.
HUYU HAPA MWANAUME
Akizungumza na mwanahabari wetu kwa tabu huku polisi wakiwa wamempiga pingu kitandani, Raphael alisimulia kwa maumivu makali:
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, SACP Leonard Paul.
“Mke wangu ni Veronica lbrahim ambaye tumeishi kwa miaka 6 na kujaliwa kupata mtoto mmoja.
“Mwezi wa tano mwaka huu, tuligombana, niliondoka nyumbani, kwa heshima ya mtoto wangu, sikuchukua kitu chochote zaidi ya nguo.
“Mwezi huohuo nilifanikiwa kuingia kwenye uhusiano na Mwalimu Rosemary ambapo baada ya penzi kukolea aliniambia nihamie kwake ili tulifaidi penzi letu tamu yaani mahaba motomoto na niliishi pale miezi mitano.”
FUMANIZI?
Alipotakiwa kuelezea chanzo cha tukio la fumanizi, jamaa alifunguka: “Hamna. Ticha aliniamsha asubuhi akaniambia nimsaidie kufanya usafi na kumuogesha mwanaye.
MADAWA YA KIENYEJI
“Nilipomaliza kumuogesha nilitaka kutandika kitanda, nilipoinua godoro niliona madawa ya kienyeji.
“Nilipomuuliza mwenzangu akawa mkali kama pilipili ndipo ugomvi mkubwa ukaanzia hapo.
“Baada ya mzozo mkali, ndugu zake walinivamia, akiwemo shemeji yangu wa kiume, namfahamu kwa jina la baba Dickson.
MAUMIVU
“Wakati najitetea, nilishika kisu ambapo katika hekaheka ya kunyang’anyana na Rosemary kilinichoma mimi na yeye.”
TICHA ARUHUSIWA
Mwandishi wetu alifika wodi namba tatu aliyolazwa ticha huyo na kuelezwa kuwa aliruhusiwa baada ya kupata nafuu ya majeraha mengi ya visu aliyoyapata sehemu mbalimbali za mwili wake hasa kichwani.
Baada ya kumkosa ticha huyo wodini, gazeti hili lilimfuata nyumbani kwake, alipobanwa alisema:
”Tukio hili limetokana na ushirikina wa mke wa zamani, alinitishia kuwa nikishika mimba nitajifungulia mdomoni akiapa kunifanyia kitu mbaya.
“Yaani hata sijui nini kimetokea, Raphael, mume wangu kipenzi amenichoma kisu na yeye kujichoma tumboni.”
KAMANDA WA POLISI
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, SACP Leonard Paul alithibitisha kutokea kwa tukio hilo.
“Tukio hilo liliripotiwa Oktoba 27, mwaka huu, ambapo Raphael alikwenda kwa mpenzi wake, Rosemary ambako kulitokea ugomvi, wakaumizana kisa wivu wa kimapenzi, hivyo tunamshikilia mwanaume huyo huku uchunguzi ukiendelea,” alisema Kamanda Paul.