Stori: Dustan Shekidele, Morogoro KATIKA
hali ya kutisha, fumanizi lililoambatana na bonge moja la mtiti
linadaiwa kujiri nyumbani kwa mwalimu ‘ticha’ wa Shule ya Msingi ya
Mafisa ‘A’, iliyopo Manispaa ya Morogoro mjini hapa aliyefahamika kwa
jina la Rosemary Mkoba kisha watu wakachomana visu.
Mume wa mtu, Raphael Bernard (33) aliyechomana visu na mwalimu baada ya fumanizi.
HABARI KAMILI Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo, msala…
Stori: Dustan Shekidele, Morogoro KATIKA
hali ya kutisha, fumanizi lililoambatana na bonge moja la mtiti
linadaiwa kujiri nyumbani kwa mwalimu ‘ticha’ wa Shule ya Msingi ya
Mafisa ‘A’, iliyopo Manispaa ya Morogoro mjini hapa aliyefahamika kwa
jina la Rosemary Mkoba kisha watu wakachomana visu.
Mume wa mtu, Raphael Bernard (33) aliyechomana visu na mwalimu baada ya fumanizi.
HABARI KAMILI Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio
hilo, msala huo ulijiri juzikati nyumbani kwa ticha huyo, Kichangani
ambapo mwalimu huyo alidaiwa kufumwa na mume wa mtu, Raphael Bernard
(33) ambaye ni dereva wa bodaboda.
ILIKUWAJE? Habari zilidai kwamba mwenye mume
amekuwa akimfuatilia mumewe kwa muda mrefu, akagundua huwa anakwenda
kujichimbia kwa ticha huyo huku akiacha familia ikilala njaa.
Ilisemekana kuwa, siku ya tukio, mwenye mume, akiwa na ‘jeshi’ lake,
alimfuatilia mumewe hadi akamuona akiingia nyumbani kwa hawara wake
huyo.
APEWA MUDA AVUTE PUMZI
Ikazidi kudaiwa kwamba baada ya kuhakikisha jamaa amelala kwa ticha
huyo, mwanamke huyo na ‘skwadi’ yake waliondoka, asubuhi iliyofuata
mishale ya saa 1:04 wakatia timu na kulianzisha timbwili huku mke huyo
akidaiwa kumtishia ticha kuwa akipata ujauzito atazaa kwa mdomo.
Bw. Raphael Bernard akiuguza majeraha hospitalini.
Habari zinadai kuwa, baada ya mke huyo na timu yake kuondoka, ticha
huyo alimuwakia Raphael kwamba kumbe ana mke, kwa nini hakuwahi
kumwambia? Ugomvi mwingine ukazuka hapo.
MASHUHUDA SASA Nao mashuhuda ambao ni majirani
wa mwalimu huyo, Juma Hamis na Joyce Joseph, walipozungumza na paparazi
wetu walisema siku hiyo walisikia vurugu kutoka ndani kwa mwalimu ambapo
walikwenda kushuhudia.
Walisema walimkuta mwanaume huyo akipigana na ticha ambaye alikuwa
akiendelea kulalamika kufichwa suala la mwanaume wake kuwa na mke.
WACHOMANA VISU “Unaambiwa mzozo huo ulipamba moto, maana yule mke aliyeondoka alidai amemfumania mumewe, mwalimu naye akadai alikuwa hajui.
“Katika purukushani hiyo huku wakipigana wao kwa wao ndipo wakachomana visu. Yaani mwanaume alijeruhiwa vibaya mno.
Mwalimu ‘ticha’ wa Shule ya Msingi ya Mafisa ‘A’ aliyechomana visu na Bw. Raphael Bernard.
“Mwanaume alichomwa kisu utumbo ukatoka nje na kama siyo polisi
kufika na kukimbizwa hospitalini, sasa hivi tungekuwa tunaimba
‘Parapanda Italia….Parapanda…’ kwani hali ilikuwa mbaya sana,” alisema
Joyce kwa masikitiko.
HOSPITALINI Baada ya kuzungumza na majirani na
mashuhuda wa tukio hilo, mwanahabari wetu alitia gia kwenye pikipiki
yake aina ya ‘boksa’ hadi Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro.
Mwandishi wetu alizungumza na Kaimu Mganga Mfawidhi, Dk. Francis Semwene ambaye alikiri kuwapokea majeruhi hao.
“Mwanaume alikuwa amepasuka tumboni hivyo tunaendelea kumpa matibabu,
yupo wodi namba moja na mwanamke ambaye naye amechomwa visu sehemu
mbalimbali za mwili wake, naye tunaendelea kumpatia matibabu,” alisema
Dk. Semwene.
HUYU HAPA MWANAUME
Akizungumza na mwanahabari wetu kwa tabu huku polisi wakiwa wamempiga pingu kitandani, Raphael alisimulia kwa maumivu makali:
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, SACP Leonard Paul.
“Mke wangu ni Veronica lbrahim ambaye tumeishi kwa miaka 6 na kujaliwa kupata mtoto mmoja.
“Mwezi wa tano mwaka huu, tuligombana, niliondoka nyumbani, kwa heshima ya mtoto wangu, sikuchukua kitu chochote zaidi ya nguo.
“Mwezi huohuo nilifanikiwa kuingia kwenye uhusiano na Mwalimu
Rosemary ambapo baada ya penzi kukolea aliniambia nihamie kwake ili
tulifaidi penzi letu tamu yaani mahaba motomoto na niliishi pale miezi
mitano.”
FUMANIZI? Alipotakiwa kuelezea chanzo cha tukio
la fumanizi, jamaa alifunguka: “Hamna. Ticha aliniamsha asubuhi
akaniambia nimsaidie kufanya usafi na kumuogesha mwanaye.
MADAWA YA KIENYEJI “Nilipomaliza kumuogesha nilitaka kutandika kitanda, nilipoinua godoro niliona madawa ya kienyeji.
“Nilipomuuliza mwenzangu akawa mkali kama pilipili ndipo ugomvi mkubwa ukaanzia hapo.
“Baada ya mzozo mkali, ndugu zake walinivamia, akiwemo shemeji yangu wa kiume, namfahamu kwa jina la baba Dickson.
MAUMIVU “Wakati najitetea, nilishika kisu ambapo katika hekaheka ya kunyang’anyana na Rosemary kilinichoma mimi na yeye.”
TICHA ARUHUSIWA Mwandishi wetu alifika wodi
namba tatu aliyolazwa ticha huyo na kuelezwa kuwa aliruhusiwa baada ya
kupata nafuu ya majeraha mengi ya visu aliyoyapata sehemu mbalimbali za
mwili wake hasa kichwani.
Baada ya kumkosa ticha huyo wodini, gazeti hili lilimfuata nyumbani kwake, alipobanwa alisema:
”Tukio hili limetokana na ushirikina wa mke wa zamani, alinitishia kuwa
nikishika mimba nitajifungulia mdomoni akiapa kunifanyia kitu mbaya.
“Yaani hata sijui nini kimetokea, Raphael, mume wangu kipenzi amenichoma kisu na yeye kujichoma tumboni.”
KAMANDA WA POLISI Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, SACP Leonard Paul alithibitisha kutokea kwa tukio hilo.
“Tukio hilo liliripotiwa Oktoba 27, mwaka huu, ambapo Raphael alikwenda
kwa mpenzi wake, Rosemary ambako kulitokea ugomvi, wakaumizana kisa
wivu wa kimapenzi, hivyo tunamshikilia mwanaume huyo huku uchunguzi
ukiendelea,” alisema Kamanda Paul.