Wednesday, 11 December 2013

Hayati Mandela aendelea kumiminiwa sifa

Mwili wa aliyekuwa rais wa kwanza mweusi wa Afrika Kusini Marehemu Nelson Mandela umewasili kwenye ikulu ya Afrika Kusini mji Mkuu wa Pretoria, na utalala hapo kwa siku tatu.
Mwili ulichukuliwa katika msafara kutoka chumba cha maiti cha hosptali hadi kwenye jengo la Muungano.
Msafara wenye jeneza la Marehemu uliondoka mjini katika Hosptali ya jeshi muda mfupi siku ya jumatano. Jeneza lilibebwa kwenye gari maalum na kufunikwa bendera ya Afrika Kusini.
Wananchi walijipanga

Kauli ya kutolipiza kisasi aliyoitoa Rais Kikwete yaibua mapya....Profesa Baregu amtaka aombe radhi kwa kuwa serikali yake imejaa visasi


KAULI iliyotolewa na Rais Jakaya Kikwete kwenye maadhimisho ya miaka 52 ya Uhuru wa Tanganyika, yaliyofanyika juzi jijini Dar es Salaam, kwa kuwataka watu wanaotaka uongozi kutokuwa na visasi imezua maswali kwa baadhi ya wasomi na wanasiasa.
 

Hatua hiyo imekuja kutokana na hotuba yake aliyoitoa kwenye maadhimisho hayo, Rais Kikwete bila ya kumtaja mtu wala chama, aliwanyooshea kidole baadhi ya wanasiasa ambao wamekuwa wakitajwa kutaka kuwania urais kwenye uchaguzi mkuu ujao.

Hivi karibuni Rais Kikwete alisema